HabariNews

Hotuba ya 1 ya Rais Kwa taifa: Je, imezima Kiu cha Wakenya kuhusu Gharama ya maisha?

Rais William Ruto hatimaye amelihutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake, hotuba ambayo ilitarajiwa kukinaisha kiu cha Wakenya kuhusu kupungua kwa gharama ya maisha.

Katika hotuba yake ya kurasa 52 na maneno 5,863, kwenye kikao cha pamoja bungeni rais alitarajiwa kupeana matumaini kwa Wakenya ambao wanaendelea kugharamikia zaidi.

Kwenye hotuba yake hiyo iliyoangazia masuala mbali mbali yakiwemo ya usalama, ufisadi, suala ya nyumba za makazi ya bei nafuu, afya huduma za vijana NYS, na japo suala la gharama ya maisha na uchumi aliligusia kwamba mikakati imewekwa.

Rais William Ruto amesema Swala la gharama ya juu ya maisha sio tatizo la kudhania bali ni tatizo lililo wazi na la uhakika linalokumba Wakenya wote nchini.

Amesema hatua muhimu za kupunguza gharama ya maisha zimetekelezwa kupitia kwa wizara ya kilimo.

Tangu siku ya kwanza ofisini, tumefanya kazi ngumu kila siku kusongesha ajenda yetu mbele, huku kukiwa na changamoto nyingi, kutengeneza njia ya kuelekea kwenye maendeleo,” alisema.

Ruto aidha ameongeza kuwa serikali yake imejitolea kupambana na suala la njaa kwa kuwekeza zaidiweka mbinu mwafaka kwenye idara ya kilimo akidokeza kuwa kupitia kupunguzwa kwa bei ya mbolea kutoka 6500-2500 kumeleta ongezeko la mazao.

Rais aidha alibainisha kuwa kuhama kwa serikali kuwekeza katika kusaidia uzalishaji wa kilimo, kinyume na kutoa ruzuku kwa matumizi, kumekuwa na matokeo ya ajabu, na kusababisha kushuka kwa gharama ya unga.

Leo pakiti ya kilo 2 ya unga wa mahindi inauzwa kwa bei ya chini ya shilingi 145 na juu ya shilingi 175 kulingana na kampuni kutoka shilingi 250. Gorogoro ya mahindi inauzwa kati ya Shilingi 60 na Shilingi 75,” alisema.

Kuhusu mpango wa Nyumba za bei nafuu, rais alisema, si tu kwamba imewezesha watu wa kipato cha chini kuwa wamiliki wa nyumba bali pia imetoa ajira kwa vijana katika ujenzi na msururu wake wa thamani.

Wakenya 50,000, ambao hawakuwa na ajira hapo awali, sasa wanahusika moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika biashara hii, “ alisema.

BY MJOMBA RASHID