Chama cha ODM kaunti ya Kilifi kimepokea jumla ya wanachama wapya 50,000 tangu kuzinduliwa kwa zoezi la usajili na kinara wa chama hicho Raila Odinga mwezi jana.
Chama hicho kimedokeza kuwa wengi wanaojiunga na chama cha chungwa ni wale wanaotoka kwenye muungano wa Kenya Kwanza wakisema wakidai kuwa ni kutokana na serikali kukosa kutimiza ahdi walizoeka wakati wa kampeni.
Mwenyekiti wa chama hicho Teddy Mwambire alieleza kuwa ODM imeendelea kupokea wanchama wapya wengine wakiwa ni wale waliohama chama hicho hapo awali.
“Hata wale walikuwa vhama pinzani wamejiunga, kwa sababu zoezi hili la usajili linaendelea idadi hii siwezi kukupa kamili kwa kuwa inazidi kuongezeka, lakini kwa sasa takribani 50,000 tayari wamingia kwa chama ndani ya Kilifi,” alisema.
Wakati uo huo Mwakilishi wa Kike kaunti hiyo Getrude Mbeyu alisisitiza kuwa idadi hiyo ingali ndogo na wanatarajia idadi kuongezeka zaidi.
Aliwasuta viongozi ambao walikihama chama hicho awali kwa tamaa zao binafsi, akikitaka chama cha ODM kuwachukulia hatua wanachama ambao anadai hawana uaminifu kwa chama, akisisitiza kuwa wasaliti hawatakubalika katika chama.
“Elfu 50 bado ni ndogo kwa Kilifi, tunataka kurudisha wanachama wetu kuna wale walitoka kwa sababu ya tamaa kwa vile vyama vingine na hawajafaulu na wanataka kurudi. Baba atakuja kuwapokea hawa lakini hatutaki moles kwa chama, tunataka wanachama waaminifu,” alisema Mbeyu.
Kauli yake iliungwa mkono na Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo ambaye amedokeza kuwa kuna uwezekano wa watu wanaojihusisha na chama hicho ilihali si wafuasi halisi wa ODM.
“Moles wako kila mahali na inaskitisha kuona waheshimiwa wengine wanasimama na kukashifu ODM na wao si wanachama, hawako katika chama. Tunawaambia waachane na chama cha ODM hakiwahusu.” Alisema.
BY NEWSDESK