HabariNews

Krisimasi tofauti; Mbwembwe na sherehe zilizo tofauti na kawaida zashuhudiwa Pwani

Waumini wa Kikiristo hapa nchini wamejumuika na waumini wengine kote ulimwenguni kuadhimisha sikukuu ya Krismasi.

Maadhimisho ya Sikukuu hii hufanyika kila mwaka Desemba 25 kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa mujibu wa imani ya dini hiyo.

Sikukuu hii imeadhimishwa tofauti na ilivyozoeleka wakati Wakenya wengi wakilalamikia gharama ya maisha, huku mbwembwe zilizozoeleka kuambatana na sherehe kama hizo hapo awali zikikosa kuonekana mwaka huu.

Wakenya wengi wamesalia mijini na kukosa kusafiri Kwenda mashambani au vijijini sawia na kutembela vituo tofauti tofauti vya burudani kutokana na ugumu wa maisha.

Licha ya baadhi ya watu kusafiri kueleka mashinani kujumuika na ndugu, marafiki na familia zao, kuna wengine ambao wameshindwa kusafiri wakilazimika kuendelea na shughuli za kawaida ili angalau kupata kipato kukidhi mahitaji yao ya kimsingi.

Mamia ya wakazi wa Mombasa wamefurika katika fuo ya bahari ya Jomo Kenyatta maarufu ‘Pirates’ kuadhimisha Sikukuu hii ya Krisimasi kwa mandhari na upepo mwanana wa baharini labda kujiliwaza na kujisahaulisha matatizo ya kiuchumi na ongezeko la gharama ya maisha inayoendelea kuwazonga.

Kwa wahudumu wa uchukuzi wa umma walisema msimu huu umekuwa mgumu ikilinganishwa na misimu mingine iliyotangulia.

“Maisha imebana watu sana, hakuna watu wengi wamefunga safari kuenda kula Sikukuu nyumbani, miaka ya nyuma ungeona mizigo mingi hapa na wasafiri,” alisema mhudumu mmoja.

“Tulikuwa tunatengeza zaidi ya elfu 10, 20 kwa siku lakini sasa hata elfu 2 kufikisha inakuwa ngumu, wengi wametulia nyumbani hawatoki na mtoto ananingojea na back to school na sina pesa hii inanishangaza,” alisema mwengine.

Viongozi wa makanisha nchini Kenya wametoa chanagamoto kwa Wakenya wenye uwezo kuwakumbuka ambao hawana kipato wakati wa kusherehekea sikukuu hiyo ya Krismasi.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri Anthony Muheria ameutaja msimu huu kuwa mwafaka wa kuonyesha ukarimu, kuwajali na kuwahurumia watu wengine kama alivyokuwa yesu Kristu.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis akihutubia Hata hivyo kwa baadhi ya wakenya waliomudu wameonekana katika sehemu kadhaa za burudani na vivutio vya watalii na wageni.

waumini mkesha wa Sikukuu hiyo, aliwahimiza waumini wa dini hiyo umuhimu wa kudumisha amani.

Papa Francis akatoa wito huo wakati wa ibada ya Sikukuu ya Krisimasi aliyoiongoza mjini Vatican, sikukuu inayojiri wakati wa msururu wa vita na mashambulizi yanayoendelea huko Ukanda wa Gaza na nchini Ukraine.

Mjini Bethlehem kunakoaminika Yesu alizaliwa sherehe za kila mwaka za Krisimasi zikafutiliwa mbali ikiwemo pamoja na shamrashamra na mbwembwe za mji mzima ambazo huwa vivutio kwa watalii.

MJOMBA RASHID NA MASHIRIKA