Uncategorized

Karo yageuka Kero Shule Zikifunguliwa

Huku shule zikitarajiwa kufunguliwa Jumatatu ya tarehe 8 Januari 2024, wazazi wameendelea kulalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kama vile vitabu, sare za shule  na huduma nyinginezo muhimu ikiwemo nauli za usafiri pamoja na karo ambayo wanadai sasa imekuwa kero.

Mwenyekiti wa muungano wa kitaifa wa wazazi nchini Silas Obuhatsa alisisitiza kwamba wazazi wengi wanapitia kipindi kigumu cha hali ya maisha na kupelekea wengi wao kutomudu karo, vifaa vya shule na gharama nyinginezo.

Kulingana na Silas, kupanda kwa gharama ya maisha kumeathiri pakubwa sekta ya elimu nchini hali ambayo ilichangiwa nakudorora kwa uchumi wa taifa.

Mwenyekiti huyo amewataka wazazi kuwapeleka wanawao shuleni licha ya hali hiyo huku akitoa wito kwa wakuu wa shule kutowatuma wanafunzi nyumbani kutokana na ukosefu wa karo.

Serikali kupitia wizara ya elimu siku ya jumatano ilitoa shilingi biloni 31 ili kufadhili masomo ya shule za msingi, sekondari ya msingi,  shule ya upili, vyuo vya kiufundi, vyuo anuai na vyuo vikuu. Pesa hizo zinadaiwa kuwa chache mno kutatua changaomoto zilizoko katika ngazi hizo tofauti za elimu.

Itakumbukwa kuwa wanafunzi 1.4 wanatarajiwa kujiunga na shule ya upili hali ambayo pia huenda ikatatiza zaidi kutokana na uhaba wa miundo msingi ya kutosha shuleni, uhaba wa walimu, ukosefu wa ufadhili miongoni mwa changamoto nyingine.

BY NEWS DESK