HabariNews

Shughuli za Ugavi wa Vifaa na Dawa kukabili Viwavi Kwale

Serikali ya kaunti ya Kwale kupitia wizara ya kilimo imezindua shughli ya ugavi wa vifaa pamoja na dawa za kukabiliana  na viwavi.

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani alisema kuwa hatua hiyo itapiga jeki sekta ya kilimo katika kaunti hiyo na kutatua tatizo la wadudu kama vile viwavi ambao wamekuwa wakiharibu mimea ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo.

Achani vile vile aliaini kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5 vitasambazwa kwa makundi ya wakulima kutoka wodi zote 20 kaunti ya Kwale ili kuwasaidia haswa wakati wa msimu wa mvua.

sisi tunakupatia hizi pembejeo ambazo zinaweza kusaidia ili tuwezekupigana vita na viwavi na wale wadudu wote ambao wanasumbua mimea yetu, kwa hivyo kama serikali ya kaunti tukishirikiana na waheshimiwa wajumbe tumenunua vitu vya milioni 4.5 ili kusaidia wakulia wetu wa wodi zetu zote 20” Alisema

BY NEWS DESK