HabariNews

Viongozi wa UDA Mombasa wamkosoa gavana Nassir kwa madai ya utepetevu.

Baadhi ya Viongozi wanaoegemea mrengo wa Serikali ya Kenya Kwanza kaunti ya Mombasa wamekosoa sera za uongozi wa gavana Abdulswamad Shariff Nassir.

Viongozi hao ambao ni wanachama wa UDA walidai kwamba gavana Nassir ameonyesha utepetevu katika utekelezaji wa tangu achaguliwe kuwa gavana mwaka 2022.

Mwakilishi wa Wadi ya Junda Sylvester Kai alidai kwamba gavana huyo amekuwa akiendeleza siasa abadala ya kuwajibikia majukumu yake ya kisheria ya kuhakikisha maendeleo yanaafikiwa katika wadi zote.

Kulingana naye, serikali inaelekea katika bajeti ya pili ya mwaka  na hakuna miradi ya maendeleo iliyoshuhudiwa.

 “I don’t know I should rate from which angle because kurate mtu ni iwe amejaribu ndio useme amejaribu asilimia hii, lakini I tell you as a matter of fact hakuna kitu ambayo mimi naweza kutumia kurate serikali hii ya Mombasa ambayo amefanyia kazi watu wa junda kazi yoyote,” alisema Kai.

Mwakilishi huo aliongeza kuwa licha ya wawakilishi wadi kujizatiti kufanikisha maendeleo mashinani, juhudi zao bungeni zinagonga mwamba kwani utekelezwaji ni finyu huku siasa zikitawala  uongozi wa kaunti hiyo.

Kwa upande mwingine kiongozi huyo aliwalaumu wawakilishi wenza wa chama cha ODM ambao ndio wengi kwa kudidimiza jukumu kuu la uangalizi wa serikali kwani hawajakuwa tayari kushirikiana nao licha ya maeneo yao pia kubaki nyuma kimaendeleo.

Kai ambaye pia ni mwanakamati wa kamati ya uhasibu wa umma katika bunge la kaunti ya Mombasa alielekeza kidole cha lawama kwa utawala akidai umeshindwa kununua vifaa muhimu kama vile taa za usalama mitaani licha ya kutengewa fedha.

“Tangu tuingi hatujafanya ile tunaita purchasing, kwa sababu tunapopurchase ndo maana tunaweza kupanua zile street light.

So what we’ve been doing tumekuwa tu tukirekebisha zile ambazo zipo.” Aliongeza Kai.

BY EDITORIAL DESK.