Makala

Fidia bwawa la maji la Mwache

Wakaazi wa vijiji vilivyolengwa kuathirika na mradi wa bwawa la maji la mwache wadi ya kasemeni kaunti ya kwale wanataka zoezi la kulipwa fidia ya ardhi yao kusitishwa hadi tume ya kitaifa ya ardhi nchini itakapoafikiana kuhusu kiwango cha fidia. 

Wanasema tume hiyo inataka kuwalipa kiwango kati ya shilingi laki mbili na shilingi lakini tatu unusu huku wakidai kushurutishwa kutia saini.

Wanadai serikali kupitia tume ya ardhi nchini inalenga kuwadhulumu kwa kuwa fidia niyachini chini ya kiwango cha thamani ya ardhi yao ya sasa.

Wanasema juhudi zao za kuwatafuta Gavana wa kwale Salim Mvurya, Mbunge wa eneo hilo Benjamin Tayari, na mwakilishi wadi Antony Yama hazijafaulu hadi sasa.

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti hiyo Zuleikha hassan anasema kuna hofu waathiriwa hao huenda wakaishi maisha ya umaskini baada ya malipo hayo, kutokana kuwa thamani ya ardhi ni zaidi ya fidia wanayopewa.

Comments (1)

  1. walipwe pesa zao kulingana na thamani ya ardhi

Comment here