Habari

Mji wa Kale kupoteza muonekano wake

Wadau wa mazingira hapa pwani wameonya uwezekano wa mji wa Kale hapa Mombasa kupoteza muonekano wake kutokana na shughuli za kisasa za kibinadam.

Katibu wa chama cha United Green Movement Hamisa Zaja anasema majengo ya kihistoria katika eneo hilo yamekuwa yakiporomoka kutokana na shughuli za ukarabati zinazoendeshwa sehemu hiyo.

Bi Zaja anasema Zana zinazotumika wakati wa ukarabati zimekuwa zikitingisha ardhi na kuchangia baadhi ya majengo kutoa nyufa na hatimaye kuanguka.

Wakati huo huo Mwanaharakati huyo wa mazingira amesema mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari kubwa katika majengo mengi katika mji wa kale, na kuwasihi wananchi kuweka mazingira bora eneo hilo.

Comment here