Habari

Ajali barabara kuu ya Mombasa -Malindi

Watoto wawili wameaga dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani eneo la  Msabaha kwenye barabara kuu ya Malindi Mombasa. 

Watoto hao wenye umri kati ya miaka 17 na 16 wamefariki wakati dereva wa lori aliyekuwa akitokea Mombasa akijaribu kupita gari dogo na kuwagonga ana kwa ana.

Kulingana na walio shuhudia ajali hiyo wawili hao walikuwa wakiendesha pikipiki kabla ya kugongwa na gari aina ya lori na kuaga dunia papo hapo.

Hata hivyo wenyeji eneo hilo walifurahishwa na juhudi za maafisa wa usalama kunusuru manusura huku ajali hiyo ikisababisha msongamano mkubwa eneo hilo.

akithibutisha kisa hicho kamanda wa polisi mjini Malindi Joe Lekuta amesema miili ya wawili hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Malindi.

Lekuta amewaonya madereva dhidi ya kuendesha magari kwa mwendo wa kasi akisema watakao patikana wakivunja sheria watatiwa mbaroni.

Comment here