MombasaSiasa

Demokrasia yachangia pakubwa mabadiliko ya mfumo wa siasa na maswala ya uongozi

Viongozi wa siasa hapa Mombasa wanasema demokrasia nchini imechangia pakubwa mabadiliko ya mfumo wa siasa na maswala ya uongozi.

Mwanaharakati wa siasa Hassan Albeity anasema ziara ya rais Uhuru Kenyatta eneo la mlima kenya huenda imechangiwa na umaarufu wake kupungua kutokana na maswala ya utendakazi.

Akizungumza katika kipindi cha Sauti asubuhi hapa sauti ya Pwani, Albeity amesema kwa muda jamii za eneo la mlima kenya zimekuwa zikionyesha umoja japo siasa za sasa huenda zinasababisha mgawanyiko.

Kuhusu vurugu za wanasiasa zinazoshuhudiwa Albeity amesema viongozi wakuu wa siasa huenda wanatumia wanasiasa wengine kusababisha mvutano hatua inayotoa picha mbaya ya saisa za taifa.

Comment here