Siasa

RUTO AANZA ZIARA YAKE HAPA PWANI HII LEO.

Naibu rais William Ruto hii leo anaanza rasmi ziara ya siku tatu katika eneo hili la Pwani, ambapo atazuru kaunti za KWALE, Kilifi na Mombasa.

Ziara ya naibu rais William Ruto ni ya kuzindua miradi mbali mbali ikiwemo kuendeleza siasa za kujipigia debe katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Leo adhuhuri RUTO anatarajiwa kuzuru eneo la Mwangulu huko lunga lunga Kwale ambapo anatarajiwa kuzindua kituo cha polisi cha Mwangulu , ambacho kilijengwa kupitisha hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge NCDF.

Hapo kesho Ruto atazuru kaunti ya Kilifi ambapo atawakabidhi pikipiki wahudumu wa bodaboda vile vile kuwakabili wanawake na makundi ya vijana vifaa vya urembo, katika mtaa wa Timboni huko Watamu.

Baadae atafanya mkutano wa hadhara kabla ya kuelekea hapa Mombasa katika uwanja wa Kadogo ambapo atazindua mradi wa kuwawezesha vijana.

Pia siku hiyo ya kesho Ruto anatarajiwa kukutana na viongozi wanaomuunga mkono katika mkutano wa faragha.

Comment here