Habari

WAHUDUMU 5 WA BODABODA WASAKWA HAPA MOMBASA BAADA YA KUMPORA DEREVA SHILINGI ELFU 500

Polisi hapa mjini MOMBASA wanawasaka wahudumu wa Boda Boda waliomshambulia na kumuibia mtu mmoja baada ya gari lake kugongana na pikipiki huko Nyali.

Inaarifiwa kwamba baada ya ajali hiyo, mtu huyo alikubaliana na mhudumu huyo wa bodaboda aliyemgonga kumlipa shilingi elfu 5.

Hata hivyo wahudumu wengine wa bodaboda walipobaini kwamba huenda mtu huyo alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha walimuandama na kumpokonya shilingi elfu 500 alizokuwa nazo.

Polisi wanasema wahudumu hao wa bodaboda walikuwa watano na kwa sasa juhudi za kuwasaka zinaendelea.

Mkuu wa idara ya upelelezi DCI George Kinoti anasema juhudi za kuwasaka wahuika zinaendelea.

Comment here