Habari

VIJANA WAITAKA SERIKALI KUONGEZA MKATABA WA UTENDAKAZI WA KAZI MTAANI.

Wakiongozwa na Habert Kinyundo vijana hao wanasema kwa sasa wamefanikiwa kuchukua mikopo kutokana na ajira hiyo hivyo kujiendeleza kimaisha.

Kinyundo anasema kuna haja ya serikali kuongeza kiwango cha fedha wanazopewa kila mwezi ili kuwawezesha kulipa malimbikizi ya madeni waliyonayo kwa sasa.

Wakati uohuo Happy Mbuche, mmoja wa vijana hao anasema serikali inafaa kuongeza mkataba wao hata Zaidi ili waweze kukimu familia zao kutia kwa ajira hiyo.

Mbuche anadai kwa sasa serikali huchelewesha malipo yao ya kila mwezi hatua anayoitaja kama changamoto kuu katika kutekeleza majukumu yao.

Serikali ilianzisha mpango huo ili kutoa ajira kwa maelfu ya vijana waliochwa solemba baada ya kampuni nyingi nchini kufunga baada ya janga la Corona kuripotiwa humu nchini Macha 2020.

Comment here