HabariUncategorized

KIJANA AAGA KATIKA ZOEZI LA MAKURUTU

Maxwell Saro, mwenye umri wa miaka 24 ameaga dunia katika hospitali moja ya kibinafsi mjini humo baada ya kudaiwa kuhisi maumivu makali usiku wa kuamki leo.

Kulingana na babake marehemu, Joseph Saro, mwanae alikuwa buheri wa afya wakati alipoenda kwenye zoezi hilo.

Anadai baada ya kushiriki mbio za masafa marefu mwanawe alianza kuhisi maumivu tumboni hatua iliyomlazimu kusitisha zoezi hilo.

Hata hivyo marehemu alipekekwa hospitalini na kupata nafuu kabla ya hali yake kugeuka gafla na kuaga dunia mapema leo.

Awali inadaiwa marehemu alidinda kupelekwa chuo kikuu na wazazi wake akiapa kujiunga na jeshi endapo angefaulu.

Joseph Yeri.
Sauti ya Pwani reporter.

Comment here