Habari

BUNGE LA KAUNTI YA LAMU LIMEPITISHA MSWADA WA KUAHIRISHA VIKAO VYAKE VYA BUNGE

Wawakilishi wadi wa bunge hilo sasa wanatarajiwa kuhudhuria semina ya wiki moja hapa Mombasa ili kupata mafunzo hayo kuhusu mswada wa ripoti ya BBI ili kuichambua na kuifahamu vyema.

Baada ya semina hiyo wawakilishi wadi watarejea mashinani ili kuhusisha na kuwaelimisha wakaazi wa lamu ili wapate kutoa maoni yao kuhusu ripoti hiyo kabla ya kuwasilishwa tena bungeni.

Siku tatu zilizopita bunge la kaunti ya Lamu liliwasilisha mswada wa BBI mbele ya bunge hilo tayari kuanza mchakato wa kuijadili sawa na kuelimisha wakaazi.

 

 

 

 

 

 

Comment here