Habari

WATU TISA WAMEFARIKI KATIKA AJALI MBAYA YA BARABARANI HUKO GILGIL

Kamanda wa oilisi Gilgil John Onditi amesema mtu mmoja amejeruhiwa katika ajali hiyo iliotokea majira ya saa kumi na moja alfajiri na yuko katika hali mahututi.

Onditi amesema ajali hiyo imehusisha gari la kampuni ya Molo Line lililokuwa likitoka Nakuru kuja Nairobi wakati lilipogongana na trela iliyokuwa ikielekea Nakuru.

Majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya St. Marys kwa matibabu huku mili ya waliofariki dunia ikipelekwa katika hifadhi ya Maiti ya Kaunti Ndogo ya Gilgil.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema trela ilikuwa ikijaribu kupita gari lengine na kugongana na matatu hiyo.

Joseph Jira

Sauti ya Pwani reporter

Comment here