HabariMazingira

KENHA yatakiwa kuweka matuta barabara ya Malindi – Lamu…..

Wito umetolewa kwa mamlaka ya kitaifa ya ujenzi wa barabara KENHA kuweka matuta kwenye barabara kuu ya malindi – Lamu

Akizungumza na wanahabari eneo la magarini mwakilishi wadi ya Sabaki Edward Kazungu Dela, amesema wanahitaji kuwekewa matuta katika barabara hiyo ili kuyanusuru maisha ya wakaazi eneo hilo wanaopoteza kutokana na ajali za barabarani.

Dele amedokeza kuwa licha ya wakaazi wengi kupoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani, serikali ya kaunti ya Kilifi imeshindwa kutatua swala hilo kwa kuwa imenyimwa uwezo wa kutekeleza majukumu hayo ya kuweka alama za barabarani pamoja na matuta huku kazi hiyo ikipewa mamlaka ya kitaifa ya ujenzi wa barabara  KENHA .

Aidha Dele ameilaumu mamaka hiyo kwa kuchelewesha uekaji wa matuta akisema huo ni utepetevu kwani wananchi wengi wanaendelea kupoteza maisha yao.