Uncategorized

Visa vya utovu wa usalama vyaongezeka Taita Taveta…

Kwingineko ni kuwa visa vya utovu wa usalama vimeonekana kuongezeka katika kaunti ya Taita Taveta, ambapo mwili wa  mwanamume moja umepatikana porini eneo bunge la Voi ukiwa na majeraha mabaya kichwani.

Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime ameitaka  idara ya usalama kwenye kaunti hiyo kujukumika kikamilifu kuhakikisha wahalifu wanatiwa mbaroni,

Mwadime aidha ameongeza kuwa kaunti hiyo haijawai kushuhudia visa vya kinyama kama hivyo na kusisistiza umuhimu wa wakaazi kushirikiana na idara ya usalama kwa kuwafichua wahalifu haswa mashinani ili kukabili hali kama hiyo mara mmoja

Mwadime aidha amesema kuna haja ya wananchi kutoa ushahidi mahaakamani ili washukiwa waweze kukabiliwa mna ,mkono mrefu wa sheria