HabariMombasa

Kampeni kuhusu vita dhidi ya dhulma za kijinsia yaanza Mombasa…

Kampeni kuhusu vita dhidi ya dhuluma za kijinsia imeanza kaunti ya Mombasa ambapo vijana wa umri wa kati ya miaka 18 hadi 24 wanapokea mafunzo kuhusu maadili mema .

Mashirika kadhaa ya kiserikali na yasiyo yakiserikali yameangazia kwa muda swala la dhuluma za kijinsia, haya yanajiri wakati ambapo visa vingi vimenakiliwa katika kaunti tofauti kote nchini.

Mafunzo haya yameandaliwa na Stretchers youth organization ambapo vijana wanaelimishwa mbinu za kupata usaidizi na hata jinsi ya kupiga ripoti.

Dickson Okong’o kutoka shirika hilo ameeleza kwanini wamechukua vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 24   akisema  mafunzo haya yamekuja baada ya ripoti kutolewa na wizara ya huduma za umma na jinsia  ambapo mwaka 2020 visa zaidi ya 5000 vilinakiliwa na ambapo vijana wanaobalehe ndio waliathirika zaidi.

By Joyce Mwendwa