HabariMombasa

Watu watatu wafariki katika ajali eneo la Kibarani…..

Watu watatu wamefariki papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kuhusika katika ajali iliyotokea mapema leo eneo la Kibarani hapa Mombasa.

Kulingana na mashuhuda ajali hiyo imehusisha matatu ya abiria ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana na lori lililokuwa likitoka maeneo ya Changamwe.

Miongoni mwa waliofariki ni dereva wa matatu hiyo, pamoja na abiria wawili.

Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya makadara, huku maafisa wa trafiki wakidhibiti msongamano katika eneo hilo.

By NewsDesk