HabariMazingiraSiasa

Serikali ya Kenya ikishirikiana na mashirika tofauti imefaulu kukabili nzige wa nyikani…

Serikali ya Kenya ikishirikiana na mashirika tofauti imefaulu kukabili nzige wa nyikani ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakulima na kuharibu mimea mashambani kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini.

Kulingana na waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa, serikali ikishirikiana na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO, limeshirikiana pakubwa kuhakikisha kwamba nzige hao wanaangamizwa.

Aidha Wamalwa ameongezea kwamba serikali iko macho na iko tatari kukabiliana na wimbi jengine la nzige iwapo litachipuka.

By Joyce Kelly