AfyaHabariMombasa

Idara ya usalama kaunti ya Kwale yawatadharisha wahubiri wa dini ya kikristo dhidi ya kulegeza masharti ya kukabiliana na msambao wa virusi vya corona.

Kamishena wa Kwale Joseph Kanyiri amewataka wahubiri hao kuzingatia masharti hayo hasa uvaaji wa barakoa kanisani.

Kanyiri ameonya kwamba huenda ukiukaji wa masharti hayo ukachangia maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake kasisi wa kanisa katoliki la mjini Kwale Harrison Mativo amewataka wakaazi kujitokeza kudungwa chanjo ya virusi vya corona.

Mativo amewahimiza wakristo kaunti hiyo kukubali kupokea chanjo hiyo ili kujikinga dhidi ya virusi hivyo.

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED