HabariMazingira

Baadhi ya maeneo Kwale kushuhudia mvua…….

Huenda baadhi ya maeneo ya kaunti ya Kwale yakaanza kushuhudia mvua za wastani kuanzia mwishoni mwa juma hili hadi kufikia wiki ijayo.

Akizunguma na waandishi wa habari, mkurugenzi mkuu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kaunti ya Kwale Dominic Mbindyo ametaja maeneo ya Matuga, Msambweni na Lunga lunga kuwa baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kupokea mvua hio.

Mbindyo ameongezea kwamba huenda maeneo mengine katika kaunti hio yakaendelea kushuhudia vipindi vya jua na mawingu.

 

By Nicky Waita