HabariLifestyleMombasa

Serikali yatakiwa kusitisha uhamisho wa walimu……

Katibu wa muungano wa chama cha walimu KNUT tawi la Mombasa Abdi Adan ametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya elimu nchini kusitisha uhamisho wa walimu kutoka shule moja hadi nyengine.

Akizungumza hapa Mombasa Adan ameeleza kughadhabishwa na baadhi ya uhamisho huo  akisema mara nyingi haufanyiki kwa njia ya usawa akisema mara nyingi walimu wanaofanya jukumu lao vyema shuleni ndio  wanaopata uhamisho wa haraka kutoka kwa shule moja hadi nyengine bila ya sababu ya kueleweka.

Hata hivyo ameiomba serikali kupitia wizara husika kusitisha uhamisho huo hata ikiwa mwalimu amehuduma shuleni kwa takribani miaka 5.

 

By Reporter