HabariMazingira

Wakaazi wa mwembe tayari katika kaunti  ndogo ya Mvita kaunti ya mombasa wanalalamikia uvundo…………..

Wakaazi wa mwembe tayari katika kaunti  ndogo ya mvita kaunti ya mombasa wanalalamikia uvundo unaotokana na uharibifu wa mabomba  ya kusafirisha maji chafu ambayo wanadai  huenda ukachangia katika kuwaletea maradhi.

Wakizungumza na meza yetu ya habari katika mahojiano ya kipekee, wenyeji hao wanasema kuwa licha ya kujaribu kupata afueni kutoka mikononi mwa serikali ya kaunti juhudi zao hazijafua dafu.

Kulingana na Rukia Suleiman ambaye ni mfanyibiashara wa kuuza chakula katika eneo hilo, uvundo huo umechangia pakubwa biashara yake kusambaratika kutokana na wateja kudinda kula katika kibanda chake wakiofia kuambukizwa ugonjwa unaotokana na uchafu.

Kwa upande wake Fasis Ashur ambae ni mwanakamati wa madrasa eneo hilo, asema kuwa kutokana na maji hayo machafu wanafunzi wa shule hiyo wanaathirika pakubwa huku wazazi wakishindwa kuvumilia uvundo  huo na kutaka kuwaondoa wanao katika shule hiyo.

Kwa sasa ametoa wito kwa serikali ya kaunti na idara husika kuwajibika ili kuwanusuru kutokana na hali hiyo mbaya .

 

BY DAVID OTIENO