HabariMombasa

Jaji Koome afungua rasmi kongamano la majaji hapa Mombasa…….

Jaji mkuu Martha Koome amefungua rasmi kongamano la kila mwaka la majaji linalofanyika hapa mjini Mombasa na kuwaleta pamoja zaidi ya majaji 300 pamoja na mahakimu.

Akihutubu wakati wa ufunguzi huo, Koome ametoa wito kwa viongozi hao wa idara ya mahakama kufanikisha kusuluhishwa kwa haraka kwa kesi ili kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani.

Wakati huo huo Koome amesema wanajaribu kila wawezalo kufanikisha kufunguliwa kwa mahakama ndogo ambazo zitasaidia katika kusuluhisha kesi ndogo ndogo pamoja na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata haki kwa wakati haswa mashinani.

By Warda Ahmed