AfyaHabari

Kenya yatakiwa kuchapisha majina ya walioiba fedha za covid 19……….

Shirika la IMF limeambia Kenya lichapishe majina ya waliofaidi kutokana na wizi wa fedha zilizotengwa kupambana na janga la covid 19 humu nchini.

IMF ambalo ni shirika la kimataifa la mikopo limeipatia serikali ya Kenya hadi mwisho wa mwezi huu kuweka wazi orodha hiyo la sivyo isitishe ufadhili wake.

Ikumbukwe kwamba mwezi mmoja baada ya kisa cha kwanza cha corona kuripotiwa humu nchini, IMF ilikuwa miongoni mwa taasisi za kimataifa zilizotoa mabilioni ya fedha ikiwa ni ufadhili wa kukwamua uchumi uliokuwa ukizorota kukabili maambukizi ya corona na miradi mingine.

Hata hivyo fedha hizo ziliishia mifukoni mwa wachache huku rais Uhuru Kenyatta akitoa ahadi kali kuhusu kuchukuliwa hatua kwa wahusika.

Mwishoni mwa mwaka uliopita pia alitaka majina ya wote waliopata zabuni katika shirika la KEMSA kuweza kuchapishwa lakini hatua hiyo haijaweza kuchukuliwa hadi kufikia sasa.

By Warda Ahmed