HabariSiasa

Rais Kenyatta kuzuru eneo la Ukambani…..

Rais Uhuru Kenyatta hii leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili katika eneo la Ukambani.

Rais ataanza ziara yake katika kaunti za Machakos na Makueni,na kumalizia kaunti ya Kitui hapo kesho.

Miongoni mwa miradi anayotarajiwa kutembelea ni ule wa maji na ule wa utengenezaji wa bidhaa za urembo na mavazi wa KIKOTEK.

Ikumbukwe tarehe 15 mwezi huu rais Kenyatta alikutana na viongozi wa ukambani katika Ikulu baada ya kulalamikia kusahaulika na serikali, na akaahidi kutembelea eneo hilo.

By Warda Ahmed