HabariNewsSiasa

Serikali yahimizwa kuimarisha usalama eneo la Eastleigh….

Mbunge wa Eastleigh Yusuf Haji na mwenyekiti wa jamii ya wafanyabiashara mtaani humo Abdullahi Ahmed wamewaongoza  wananchi na wafanyabiashara   kuishinikiza serikali kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Yusuf Haji amesema kuwa ameshirikiana na serikali ya kitaifa kuhakikisha  wameekeza zaidi katika maswala ya usalama kwa kuwaajiri maafisa wapya.

Wakati huo huo Abdullahi Ahmed amesema  watashirikiana  na asasi za usalama kuhakikisha kuwa uhalifu ambao umekithiri mtaani Eastleigh umemalizika na kwa wakati huo akaishukuru idara ya usalama kutokana na juhudi zake .

Haya yanajiri siku chache baada ya wahalifu waliomteka nyara Hafsa Mohammed kukamatwa katika eneo la Kinangop.

By Allan Preston