HabariSiasa

Wafuasi wa RUTO wasema hawatishwi na muungano katika ya ODM na Jubilee…..

Wanasiasa wanaomuunga mkono mkono naibu rais William Ruto kutoka eneo la bonde la ufa  wanasema  hawatatishwa na muungano kati ya chama cha jubilee na ODM.

Wakiongozwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei, viongo zi hao wanasema kwamba chama cha Jubelee kimesambaratika na kwamba kwa sasa chama hicho kimesalia mahame.

Akizungumza katika hafla ya kuwawezesha kina mama kujiinua katika miradi tofauti kwenye eneo la Cheptirit, Cherargei aidha amewataka wakereketwa wa BBI kukubali uamuzi wa mahakama.

By Nicky Waita