HabariMombasaNewsSiasa

Wanawake wahimizwa kuwania nyadhfa za uongozi bila uoga……..

Mgombea wa kiti cha ubunge eneo la Nyali Millicent Odhiambo ametoa wito kwa wanawake wa maeneo ya pwani haswa hapa Mombasa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi serikalini akisema wengi wao wameonekana kukosa motisha wa kuwa viongozi.

Katika mahojiano ya kipekee, Odhiambo amewataka wanawake kujitosa kwenye siasa bila kuogopa kwani wanawake wakiwa uongozini mahitaji ya jamii huangaziwa zaidi ikilinganishwa na wakati uongozi ni wa wanaume pekee.

Wakati huo huo, Odhiambo ameeleza kuwa mojawapo ya changamoto ambazo hufanya wanawake wengi kutowania nyadhfa za uongozi ni kwamba siasa humu nchini huhusishwa na vita, zinagharimu mamilioni ya pesa na vile vile vyama vya kisisasa mara nyingi huongozwa na wanaume.

Haya yanajiri huku wanawake wengi wakionekana kujitosa katikaulingo wa kisiasa tukielekea uchaguzi mkuu ujao.

By Caroline Nyakio