HabariMombasaNews

Familia huko Oldtown yalilia haki baada ya jamaa yao kutekwa nyara jana jioni…..

Familia ya Abdulhakim Sagar inalilia haki baada ya mwanawao huyo kutekwa nyara na watu ambao kulingana nao walikuwa maafisa wa polisi katika eneo  la Old Town alipokuwa anaeleka kuswali swala ya jioni hapo jana.

Kulingana na ndugu yake Abdul, hili ni tukio la pili yeye kutekwa nyara la kwanza   likitendeka mwaka wa 2018, ambapo baadaye  alifikishwa mahakamani kwa madai ya kujihusisha na ugaidi lakini aliachiliwa huru baada ya kukosekana ushaidi wa kutosha.

Naibu Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la HAKI AFRICA, Salma Hemed ametaka asasi za kiusalama zikiongozwa na waziri wa usalama  wa ndani Fred Matiang’i kuweka wazi ni nani  hasa aliyemteka nyara kwa sababu  kuna madai kuwa kikosi cha polisi cha kupambana na  ugaidi kilihusika na utekaji nyara huo.

By Allan Wandera