HabariMombasaNews

Kamati ya seneti yakagua miradi tofauti hapa Mombasa…….

Kamati ya miundomsingi, uchukuzi pamoja na ujenzi wa barabara katika bunge la seneti inaendelea kukagua miradi mbali mbali katika kaunti hii ya Mombasa.

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake ambae pia ni seneta wa kiambu kimani wamatangi inaendelea kusikiliza malalamisha ya wakazi wa Buxton katika bunge la kaunti ya mombasa ambao wametoa malalamishi ya kufurushwa pasi na kufuatwa kwa sheria jambo ambalo wamedai kuwa ni ukiukaji wa sheria.

Waathiriwa hao wanalalamikia kurushwa bila maelewano kati yao na msimamizi wa ujenzi wa mradi huo wa Buxton ,bei ghali ya nyumba hizo ikizingatiwa kwamba wengi walioishi hapo takriban miaka 40 hawana uwezo wa kulipa nyumba hizo miongoni mwa changamoto nyingine.

Kamati hiyo inanuia kukagua miradi mbali mbali hapa kaunti ya mombasa  ikiwemo mradi wa ujenzi daraja la liwatoni,ujenzi wa makupa by pass , barabara kuu ya changamwe, dongo kundu miongoni mwa miradi mengine.

By David Otieno