HabariNews

Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa TUM kimekabidhiwa ukumbi uliofanyiwa marekebisho….

Chuo kikuu cha kiufundi cha Mombasa TUM kimekabidhiwa ukumbi uliofanyiwa marekebisho.

Katibu mkuu wa utafiti na masomo katika vyuo vikuu nchini Simon Nabukwesi ameukabidhi usimamizi  wa chuo hicho rasmi ukumbi ambao utatumika na wanafunzi kwa maswala ya kuboresha talanta na vipaji .

Katika shughuli hiyo Nabukwesi amesema kuwa majengo katika vyuo yanapaswa kufanyiwa marekebisho ili yawe nadhifu na yakuvutia.

Kulingana na naibu kansela chuo hicho Leila Abubakar jingo hilo lilikuwa limesahaulika kwa sababu ya kupata athari ya miakana kurekebishwa kwake ni jambo la maana sana kwa chuo hicho.

BY NATASHA TALU