HabariNewsSiasa

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya ili kujadili mwelekeo wa chama cha Jubilee…

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya ili kujadili mwelekeo wa chama cha Jubilee na kujua hatma ya katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju pamoja na naibu mwenyekiti wa chama hicho David Murathe.

Katika mkutano huo rais Kenyatta amewaeleza viongozi  hao hatua ya chama hicho kuja pamoja katika kuunda muungano na chama cha ODM

Vile vile muktano huo unalenga kuimarisha chama hicho ambacho kwa sasa kinaonekana kusambaratika kwa kiwango kikubwa kutokana na utofauti ulioko baina ya rais kenyatta na naibu wake William Ruto.

BY DAVID OTIENO