HabariMazingiraMombasaNews

Mwanamke mwenye umri wa miaka 32 pamoja na mwanawe wa miaka miwili wafa maji Kwale

Mwanamke mwenye umri wa miaka 32 pamoja na mwanawe wa miaka miwili wamekufa maji baada ya kusombwa katika mto mwavumbo eneo la Kinango kaunti ya Kwale.
Mwendazake kwa jina Umazi Medza Kengo na mwanawe Kachimizi Dalu wamekumbana na mauti hapo jana walipokuwa wakivuka mto huo baada ya kutoka kanisani.
Akithibitisha kisa hicho OCPD wa eneo hilo Fredrick Ombaka amesema shughuli za kuitafuta miili hiyo bado zinaendelea.
Haya yanajiri siku chache tuu baada ya watoto watatu kufa maji katika mto huo huku mwili wa mtoto mmoja ukiwa bado haujapatikana.