HabariNewsSiasa

Sasa ni ramsi kwamba Muungano wa One Kenya Alliance unamilikiwa na vyama tanzu vya; Wiper, Kanu, Narc-Kenya na UDP.

Sasa ni ramsi kwamba Muungano wa One Kenya Alliance unamilikiwa na vyama tanzu vya; Wiper, Kanu, Narc-Kenya na UDP. Hatua hii imefuatia mkutano wa vinara wa vyama hivyo, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Gideon Moi wa KANU, Cyrus Jirongo wa UDP na Martha Karua wa Nark Kenya kukutana na kutia saini mkataba wa maelewano. Aida, Moi ametangaza mikakati ya OKA ambayo inajumuisha mikutano ya hadhara kote nchini pamoja na kampeni za kuwahamasisha wananchi kuhusu muungano huo huku akisema kwamba wako huru kuungana na vyama vingine vya kisiasa ambavyo vina maono sawa na wao. Viongozi hao wamefutilia mbali uwezekano wa kuungana na muungano wa Kenya Kwanza unaoogozwa na William Ruto.