AfyaHabariNews

Wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya coast general wanaendelea kuhangaika baada ya shughuli za matibabu kusitishwa kufuatia mgomo wa madaktari.

Baadhi ya wagonjwa hao wameeleza meza yetu ya habari kuwa hawakuwa na habari kuhusu mgomo huo huku wakisema mgomo huo umewaathiri pakubwa kwani wamekosa njia mbadala ya kufikia huduma za matibabu.
Vile vile wamedokeza kuwa hospitali ya coast general ndiyo imekuwa tegemeo lao kwani wanapata kutozwa ada rahisi ikilinganishwa na hospitali zingine.