Habari

Usimamishaji kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kwale-Kinango.

Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza amesema kusimamishwa kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kwale-Kinango kumetokana na ukosefu wa fedha. Kulingana na Tandaza, serikali ya kitaifa haijaweza kumlipa mwanakandarasi anayesimamia mradi huo utakaogharimu takriban shilingi billioni 4. Mbunge huyo amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ya urefu wa kilomita 29 ulitarajiwa kukamilika kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Wakati huo huo, Tandaza pia amedokeza kwamba barabara ya Marere-Tiribe-Kilulu imeathirika baada ya serikali kutoa kandarasi hiyo kuchelewa.

>> News Desk…