Habari

Idara ya watoto imewaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia watoto.

Idara ya watoto katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale imewaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia vibaya watoto katika kampeni zao.
Afisa wa idara hiyo Zefaniah Apoko ametoa onyo hilo linalolenga kuzuia visa vya dhulma za watoto wakati huu wa siasa.
Apoko aliyekuwa akizungumza katika eneo la Diani, amewataka wazazi kuwalinda wanao ili wasiweze kudhulumiwa na wanasiasa.
Kwa upande wake afisa wa idara ya maswala ya jinsia kaunti ya Kwale Nelly Amoite amesema kuwa huenda visa vya dhulma za watoto vikaongezeka wakati huu wa uchaguzi.
Hata hivyo, Amoite amedokeza kwamba tayari idara hiyo imezidisha hamasa za kukabiliana na visa hivyo katika jamii.

>> Editorial Desk…