HabariNewsSiasa

Idara ya usalama kaunti ya Kwale wametakiwa kuimarisha hali ya usalama katika soko la Kombani.

Idara ya usalama kaunti ya Kwale wametakiwa kuimarisha hali ya usalama katika soko la Kombani kutokana ongezeko la visa uhalifu eneo hilo.

Akizungumza na wanahabari baada ya kulikagua soko hilo, Achani ameelezea kusitishwa kwake na ongezeko la visa vya wizi na uharibifu wa mali ya umma katika soko hilo.

Gavana huyo ameitaka idara ya usalama kuwajibika katika majukumu yake ili kuhakikisha wafanyibiashara wa soko hilo wanafanya shughuli zao kwa amani.

Kwa upande wake kamanda wa polisi kaunti hiyo Josphat Kinywa ameahidi kukabiliana na visa vya utovu wa usalama katika soko hilo.

Kinywa ametaka mzozo wa malipo uliopo baina ya mwanakandarasi aliyesimamia mradi wa ujenzi wa soko hilo na serikali ya kaunti kutohitilafiana na hali ya usalama.

BY EDITORIAL DESK