HabariNews

Mashirika ya kutetea haki za binadam hapa Mombasa wameitaka serikali kuongeza juhudi za kukabilaina na makundi ya vijana.

Mashirika ya kutetea haki za binadam hapa Mombasa wameitaka serikali kuongeza juhudi za kukabilaina na makundi ya vijana wanaovamia na kuwajeruhi wananchi eneo la Kisauni.

Afisa wa dharura katika shirika la Muhuri Francis Auma, anasema vijana hao wamekuwa wakitekeleza visa hivyo bila hofu licha ya kuwa na polisi waliopitia mafunzo ya kukabili wahalifu.

Auma anasema iwapo vijana hao hawatadhibitiwa huenda hali ya usalama Mombasa ikazidi kuwa tete hat ana zaidi.

Afisa huyo amesema anahisi polisi wamezembea kazini hasa baada ya maafisa wengine kuonekana wakiandamwa na idara ya mahakama kutokana na tuhuma visa vya watu kuawa katika njia tatanishi.

Kauli ya Shirika la MUHURI inajiri saa chache baada ya mwanamke mmoja kujeruhiwa kwa panga vile vile kuibiwa mali yake na vijana hao eneo la Kisauni Mapema Leo.

BY EDITORIAL TEAM