HabariNews

Baa la Njaa laendelea kutikisa wakaazi wa Kinango -kwale.

Takwimu kutoka Serikali ya kitaifa pamoja na shirika la msalaba mwekundu wanasema takriban wakaazi laki mbili wa kaunti ya kwale wameathirika na ukame.

Maeneo yaliyoathirika zaidi na ukame unaosbabishwa na hali ya kiangazi katika kaunti hiyo ni Kinango.

Inaarifiwa kuwa vyanzo vya maji katika eneo hilo vimekauka.

Hata hivyo kunataarifa kwamba baadhi ya familia zimesambaratika kutokana na makali ya njaa, wanandoa wakilazimika kutengana na kuelekea maeneo ya Ukunda, Likoni na hapa Mombasa ili kujiendeleza.

Shirika la kijamii la Sauti ya Jamii eneo hilo likiongozwa na mwenyekiti Geoffrey Jeffa linasema wanandoa wanatalakiana kutokana na ugumu wa maisha.