HabariNews

Hatua Salim Mvurya kutaka shughuli za kuogelea kusitishwa kufikia mwendo wa saa kumi na moja jioni yakosolewa.

Wahudumu wa fuo ya bahari ya Neptune katika kitengo cha uendeshaji mashua kaunti ya Kwale wameikosoa hatua ya waziri wa madini na uchumi Samawati nchini Salim Mvurya kutaka shughuli za kuogelea kusitishwa kufikia mwendo wa saa kumi na moja jioni kuwa hatua hio inalenga kuwafungia nafasi ya kujitafutia mapato msimu huu wa sherehe.

Wakiongozwa na Ali Omar Njama wanasema kwamba shughuli za bahari zinaendeshwa kulingana na hali ya mawimbi baharini ila sio masaa ,akiitaja marufuku hio kuwa kikwazo kikuu cha shughuli zao.

Wahudumu hao wameafiki kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia sheria zilizopo za usalama wa wageni na wenyeji wanaozuru fuo hio hivyo kumtaka waziri Mvurya kuondoa marufuku hio ili kuwapatia nafasi nzuri ya kutafuta fedha za kukidhi mahitaji ya familia zao.

BY EDITORIAL DESK