HabariNews

Viongozi katika kaunti ya Kwale watakiwa kuwafanyia wananchi kazi kwani msimu wa siasa umeisha.

Viongozi wa dini katika kaunti ya Kwale wamewataka viongozi waliochaguliwa mwaka uliopita kuwafanyia wananchi kazi kwani msimu wa siasa umeisha.

Kulingana na Sheikh Amani Hamisi kutoka baraza la kidini la Inter Religious Council kaunti ya Kwale amesema kuendeleza maswala ya kisiasa kwa sasa ni kurejesha nyuma maendeleo.

Sheikh Hamisi amewataka viongozi ambao hawakupita katika uchaguzi wa mwaka uliopita kushirikiana na viongozi waliopita katika uchaguzi na kusubiri miaka mitano ijayo ili kufanya siasa za ushindani.

Ameongeza kuwa wakati wa ushindani umeisha na kila mtu aangalie anapoweza kufanya maendeleo ili kuchangia katika ukuzaji wa jamii.

BY EDITORIAL DESK