HabariNews

WAZAZI WAHIMIZWA KUWACHUNGA WANAO WAKATI HUU AMBAPO SHULE ZIMEFUNGWA.

Wazazi kaunti ya Kilifi wamehimizwa kuwashughulisha na kufuatilia nyendo za wanao hasa wakati huu ambapo wanafunzi wako likizo baada ya kutamatika kwa muhula wa kwanza.

Wanafunzi wakiendelea kupumzika nyumbani kufuatia shule kufungwa kutokana na muhula wa kwanza kukamilika, wanafunzi wametakiwa kuwa makini na kujiepusha na mienendo mibaya inayoweza kuwasababishia matatizo.

Diwani wa Mnarani Juma Chengo, amewataka wanafunzi kujiepusha na vishawishi vya utumizi wa mihadarati, licha ya upatikanaji wa baadhi yake kuwa rahisi.

Ameongeza kuwa wazazi wanafaa kuwa makini na kujukumika kwa kufuatilia nyendo za wanao ili kuwaepusha kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.

Aidha amewataka wazazi kuwashughulisha hata kwenye kazi za shamba wakati huu ambapo mvua inaendelea kushuhudiwa maeneo mengi kaunti ya Kilifi, huku akiwataka wazazi kukoma kukiri kushindwa kuwadhibiti wanao kitabia.

BY ERICKSON KADZEHA