HabariNews

Mbunge wa Magarini apoteza Kiti chake cha Ubunge

Mahakama ya Rufaa mapema leo imetupilia mbali Ombi la mbunge wa Magarini Harrison Garama Kombe kutaka kubatilisha uamuzi wa kuufuta kuchaguliwa kwake uliotolewa na Mahakama kuu mapema mwaka huu.

Mahakama hiyo aidha imeshikilia kuwa uchaguzi huo haukuandaliwa Kwa njia ya huru na uwazi ikisema zoezi hilo liligubikwa na visa vingi vya udanganyifu.

Vile vile cheti kilichopewa mbunge huyo kimefutiliwa mbali na kuagizwa kuandaliwa upya Kwa zoezi la uchaguzi eneo bunge hilo.

Stanley Kenga Karisa aliyegombania kiti hicho Kwa tiketi ya UDA alielekea mahakamani kupinga matokeo hayo akidai uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

Macho yote sasa yanaelekezwa kwa Mbunge huyo endapo ataelekea katika Mahakama ya upeo ama ataridhia matokeo hayo na kurudi debeni.

BY EDITORIAL DESK