HabariLifestyleNews

Zaidi ya Wapemba elfu 7 waishio Pwani Wapata Uraia wa Kenya.

Shangwe na nderemo zimetawala Wananchi takribani elfu 7 kutoka jamii ya Wapemba wanaoishi maeneo mbalimba ukanda wa Pwani, baada ya Rais William Ruto kuwakabidhi vyeti vya uraia wa Kenya.

Zoezi hilo ambalo limefanyika Ijumaa tarehe 28 Julai katika Uwanja wa Karisa Maitha kaunti ya Kilifi ambapo jamii hiyo ilipokezwa stakabadhi rasmi za uraia.

Stakabadhi hizo ni pamoja na vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa, hatimiliki na pasipoti kutoka kwa rais William Ruto na kutambuliwa kama Wakenya rasmi.

Kusema kweli leo ni furaha tu juu ya furaha tuliyo nayo mpaka watoto wetu kwa sababu tulikuwa tumekwama kwenye pingamizi tele,” akasema mmoja wa jamii hiyo.

Jamii hiyo imetaja hatua hiyo kuwa ya manufaa kwao huku wakisema kuwa litawasidia pakubwa kupata ajira katika taasisi za kiserikali na mashirika mengine hapa nchini.

Baadhi ya walionufaika na uraia huo wameeleza hisia zao wakitaja kama ndoto iliyotimia.

Ilikuwa shida kubwa sana majumbani tulikuwa hatukai kwa raha mara askari hawa wamefika ila leo changamoto vile imetatuliwa tunaskia raha sana. Mimi nina furaha sana leo kwa sababu ilikuwa ndoto ambayo tumeisubiria kwa hamu.”