HabariNews

Magari ya Mizigo Yapigwa Marufuku Kutumia Barabara Kuu Kaunti ya Mombasa

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amepiga marufuku magari yanayobebea mizigo mizito dhidi ya kutumia baadhi ya barabara kuu jijini Mombasa.

Akihutubia Chama cha Walipa Mikopo na Wakaazi wa Kaskazini mwa Pwani NCRRA, mnamo Ijumaa Tarehe 4 Agosti, Gavana Nassir alisema hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa magari hasa nyakati za shughuli nyingi za barabarani.

Nassir ameeleza kuwa magari yote yenye uzito wa zaidi ya tani 10 yatawekewa nyakati maalum za kupita barabara mbalimbali ikiwemo katika daraja la Nyali, barabara ya Fidel Odinga na hata barabara inayoelekea katika kivuko cha Ferry.

“Moja ya mambo ambayo yatatusaidia kupunguza msongamano ni kuweka sheria za nyakati maalum kwa magari ya mizigo, hivyo tutapunguza safari za magari hayo katika barabara ya daraja la Nyali, Barabara ya Fidel, Nyali Links, ya Kivuko cha Ferry magari hay ani yaliyozidi uzito wat ani 10.” Alisema Gavana Nassir.

Aidha magari hayo hayataruhusiwa kutumia Barabara Kuu mpya na ya zamani ya Mombasa Malindi, zamani ya Mombasa Malindi nyakati za asubuhi kati ya saa kumi na mbili na saa tatu asubuhi, kisha kuzuiwa teana kuanzia saa tisa unusu alasiri hadi saa mbili usiku.

BY EDITORIAL DESK