HabariNewsTechnology

Washukiwa 2 watiwa Mbaroni kwa Uharibifu wa Mali ya KPLC

Kufuatia oparesheni inyoendelea ikilenga waharibifu wa miundombinu ya umeme, washukiwa wawili wametiwa mbaroni na maafisa wa upelelezi baada ya kupatikana na vifaa vinavyomilikiwa na kampuni ya usambazaji umeme nchini KPLC.

Jennifer Njeri mwenye umri wa miaka 46 na William Mwangi wa miaka 26 walitiwa nguvuni katika kampuni inyojihusisha na uuzaji wa vyuma kuukuu ya Busman Investments mjini Kitengela, Kajiado.

Haya yanajiri baada ya wakenya kushuhudia ukosefu wa nguvu za umeme katika sehemu mbali mbali nchini jambo lililopelekea wakenya wengi kunyooshea kidole cha lawama KPLC.

Washukiwa hawa walipatikana na umiliki wa nyaya za umeme, fuzi, swichi za transfoma miongoni mwa vifaa vingine vinavyoaminika kuharibiwa awali.

Hata hivyo washukiwa hawa watafikishwa mahakami  Agosti 28,2023 kujibu mashtaka yanayowakabili.